Mkopo wa Elimu

Mkopo wa Elimu  huu ni mkopo kama mikopo mingine utatolewa kwa mkopaji kwa ajili ya shughuli za kielimu kama kulipia karo za shule na kununua mahitaji ya Elimu pale utakapohitajika, kiwango cha juu cha Mkopo ni Tshs 4,000,000/= muda wa marejesho hautazidi miezi kumi na mbili (12) na riba yake ikiwa asilimia 1.2. Marejesho ya mkopo huu yatafanyika kupitia makato ya mshahara wa mkopaji.