Mkopo wa Dharura
Mkopo wa dharura upo mahususi kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya dharura mbalimbali yanayoweza kumpata mwanachama wakati wowote.
Mwanachama hupewa mkopo huu wakati wowote anapokuwa ameomba kwa kujaza fomu. Riba ya mkopo huu ni asilimia 1.2, kima cha juu cha mkopo huu ni tshs 3,000,000/=ambao marejesho yake ni hadi miezi sita (6).
Marejesho ya mkopo huu yatafanyika kupitia makato ya mshahara wa mkopaji.
