Historia ya Tanesco Mbeya Saccos Ltd.

 

TANESCO Mbeya SACCOS LIMITED ni Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha wafanyakazi waajiriwa wa kudumu na Muda maalumu (TMP) wa shirika la Umeme Tanzania TANESCO. Ushirika huu ulianzishwa rasmi mnamo Mwaka 1999 ukiwa na wanachama wapatao 50. Ushirika huu umesajiliwa kwa mujibu wa sheria Ushirika namba 15 ya mwaka 1991 fungu la 30 na kupata Hati ya usajili mnamo Tarehe 18/3/1999 yenye namba-MBR 445.

Kufuatana na mabadiliko ya mara kwa mara ya sheria ya vyama vya ushirika hivi sasa chama kinafanya shughuli zake chini ya Sheria ya vyama vya ushirika Na.6 ya Mwaka 2013 na kanuni za SACCOS za mwaka 2015.
Mnamo mwezi January mwaka 2021 Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo TANESCO Mbeya SACCOS kilipewa leseni ya utoaji wa Huduma ndogo za fedha Namba MSP3-TCDC/2021/0041 Chini ya kifungu namba 20 cha sheria ya huduma ndogo za fedha ya mwaka 2018.