Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Faida juu ya akiba za mwanachama ni matumizi kutokana na bajeti ya mapato na matumizi ya mwaka husika

Mgao huo hufanywa kulingana na akiba anazomiliki mwanachama. Ikiwa chama kinataka kukuza mtaji au kuwekeza rasilimali, kiasi hicho cha mgao kitaongezwa kwenye akiba za mwanachama,. Hivyo basi chama kimekuwa kikitoa gawio kwa kila mwanachama na kuziongeza katika akaunti ya akiba ya kila mwanachama kwa kila mwisho wa mwaka wa fedha wa chama.

  • Kwa mujibu wa masharti ya chama kipengele cha 28(3) akiba za lazima haziwezi kurejeshwa au kupunguzwa kwa mwanachama isipokuwa tu uanachama unapokoma.
  • Amana ya kawaida inaweza kurejeshwa kwa mwanachama bila hata uanachama wake kukoma, kwa kuzingatia  masharti ya chama

Mwanachama ataweza kujua mwenendo wa malipo yake ya mkopo kwa kuangalia kwenye jedwali la ulipaji wa mkopo (loan repayment schedule). Jedwali hili lina taarifa za kiasi cha mkopo ulioomba,makato kwa mwezi,muda wa marejesho na kiasi cha riba katika kila rejesho kulingana na aina ya mkopo kupitia kwenye tovuti yetu .

Ndiyo.

  • Mwanachama anayetaka kupunguza deni kwa kulipa sehemu ya mkopo alionao katika chama, atatakiwa kuandika barua ya kusudio hilo kwenye chama na katika barua hiyo atataja kiasi ambacho anataka kulipa kisha ataruhusiwa kufanya hivyo na atapewa nambari ya akaunti ambayo atatakiwa kuingiza fedha hizo benki na kisha kuwasilisha hati ya malipo katika ofisi za chama na atapunguziwa riba.

  • Mwanachama atatakiwa kuandika barua ya kusudio la kulipa kwa mwenyekiti wa chama
  • afisa mikopo atakokotoa kiasi cha deni lililosalia
  • Mwanachama ataruhusiwa kufanya hivyo na atapewa nambari ya akaunti ambayo atatakiwa kuingiza fedha hizo benki
  • Na kupunguziwa riba

  • Utaratibu ni kwamba mwanachama atawasiliana na chama na kueleza nia yake ya kulipa mkopo alionao kutoka taasisi nyingine,kisha afisa mkopo hukokotoa uwezo wa mkopo ambao mwanachama atakuwa na uwezo wa kuulipa kisha hushauriwa kuleta uthibitisho wa bakaa ya mkopo alionao kutoka taasisi nyingine.kisha taratibu nyingine hufuata.ikumbukwe kuwa wajibu wa chama ni kumsaidia mwanachama kwa kumpa ushauri na namna ambayo atalipia mkopo mwingine kwa kuchukua mkopo kutoka saccos.

Mwanachama aliyechangia chama kwa muda usiopungua miezi mitatu.

  • Kuwa na mdhamini wa mkopo ni hitaji la kisheria
  • Kazi ya kinga ya mkopo kwa mujibu wa sera ya mikopo ni kinga  dhidi ya bakaa ya mikopo itakayokua imeachwa na wanachama waliofikwa na aidha mauti/kufariki au mwanachama aliepatwa na ulemavu wa kudumu na kushindwa kufanya kazi.
  • Pale mwanachama anaposhindwa kurejesha mkopo kwa sababu zingine tofauti na hizo juu, mdhamini anawajibika kusaidia kufanikisha marejesho ya mkopo huo.

  • Chama kina mfumo laini kwa kutumia “mobile app “ambapo wanachama wataweza kuingia kwenye mtandao na kupata taarifa zake.
  • Mwanachama atawezeshwa kupakua app hiyo na kupata statement zake za mikopo na michango