AMANA YA MUDA MAALUMU

Ni akaunti ya muda maalumu inayokupa riba nzuri kwa kipindi utakachotunza fedha zako na kusaidia kuweka akiba ya muda ya kipindi maalumu kulingana na malengo yaliyopangwa.

SIFA NA VIGEZO VYA AKAUNTI HII

  • Amana inawekwa kwa kipindi maalum
  • Mwanachama atapata riba itakayolipwa kila Mwezi na anaweza kuichukua faida yake.
  • Mwanachama hataruhusiwa kutoa Amana yake hadi muda utakapoiva
  • Kipindi cha mawekezo ni kuanzia 6,12,24,36
  • Mwanachama atakayevunja mkataba  wake kabla ya kufika kikomo atapoteza riba yote
  • Baada ya kujaza mkataba Utakabidhiwa risiti  ya amana yako ya muda maalum

 

MAOMBI

  • Muombaji anatakiwa kuwa mwanachama wa Tanesco Mbeya Saccos
  • Atajaza fomu na mkataba utakaopatikana ofisi za chama  

FAIDA ZA AMANA YA MUDA MAALUM (FIXED DEPOSIT)

  • Riba kubwa ya kishindani
  • Uhakika wa kupata faida ya uwekezaji kwa kipindi utakachowekeza
  • Ina Vipindi tofauti unavyoweza kuchagua kuwekeza
  • Unaweza kuwekeza kwa miezi sita, 12 au zaidi ya miaka miwili (mpaka miaka mitatu)
  • Unaruhusiwa kuongeza kiasi cha uwekezaji kadri uwezavyo kwa muda tofauti
  • Fedha za mteja zipo salama wakati wote
  • Hakuna makato ya kila mwezi