AMANA YA KAWAIDA

  • Ni akaunti ya mawekezo ya mwanachama  ambapo Mwanachama anafungua kwa ajili ya malengo tofauti tofauti na anaweza Kutoa pesa kila mara anapohitaji.
  • Mwanachama anaweza kuweka kila mwezi au mara kwa mara kulingana na malengo atakayokuwa nayo.

      FAIDA ZA MAWEKEZO YA AMANA YA KAWAIDA

  • Utapokea faida kila mwezi.
  • Riba kubwa ya kishindani.
  • Uhakika wa kupata faida ya uwekezaji kwa kipindi utakachowekeza
  • Inakupa nafasi ya kuchagua muda wa kuwekeza kwa mahitaji yako mwenyewe.
  • Unaruhusiwa kuongeza kiasi cha uwekezaji kadri uwezavyo kwa muda tofauti.
  • Fedha za mteja zipo salama wakati wote
  • Hakuna makato ya kila mwezi.

SIFA NA VIGEZO VYA AKAUNTI HII

  • Amana inawekwa  mara Kwa mara Amana itaweza kuchukuliwa
    pindi mwanachama atapohitaji
  • Amana itapata faida kila mwezi
  • Amana inaweza kukatwa kwenye mshahara au kwa malipo
    ya fedha taslimu

MAOMBI

  • Muombaji anatakiwa kuwa mwanachama wa Tanesco Mbeya
    Saccos
  • Atajaza fomu itakayopatikana ofisi za chama